BALOTELL NDIYE ANAEONGOZA KWA KUBAGULIWA ENGLAND.
>>Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ndiye mchezaji aliye baguliwa sana katika ligi ya
Uingereza ,huku mchezaji huyo akipokea zaidi ya jumbe 8000 ,asilimia 50 zikiwa ni za kibaguzi.
Takwimu hizo za kushtua zimeripotiwa na Kick it Out ,ambao walibaini kwamba raia huyo wa Itali
alilengwa sana katika mitandao ya Twitter huku mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck akipokea
jumbe 1700 asilimia hamsini zikiwa za kibaguzi.
Mshambuliaji mwenza wa Balotelli katika kilabu ya Liverpool Daniel Sturridge pia alionekana kulengwa
katika mitandao ya kijamii baada ya kupokea jumbe 1600 asilimia 60 ikiwa ni ujumbe wenye mwelekeo wa kijinsia.
Utafiti huo pia umebaini kwamba kilabu ya Chelsea ndio kilabu iliobaguliwa zaidi kwa jumbe 20,000 huku liverpool ikiwa ya pili na jumbe 19,000 Arsenal ikiwa ya tatu kwa jumbe 12,000 huku Manchester City na Manchester united zikipokea ujumbe 11,000.
.
# Source_BBC.
No comments: