Recent Posts

NEWS: CHADEMA YAPATA MBABE WA ZITTO KIGOMA KASKAZINI

CHADEMA YAPATA MBABE WA ZITTO KIGOMA KASKAZINI.

>>JIMBO la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma limepata mbadala wa kuliwakilisha Jimbo hilo
katika Uchaguzi ujao kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Zitto Kabwe kufukuzwa
katika chama hicho.

Kabla ya Zitto Kabwe kufukuzwa CHADEMA aliliwakilisha Jimbo hilo kwa Miaka Kumi sasa baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kuchaguliwa tena mwaka 2010, Lakini baada ya CHADEMA kumfukuza, Chama kimempa dhamana Mjumbe wa Kuchaguliwa Kamati Kuu Taifa
Dr. Yared Fubusa kuchukua nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka huu (2015).

Dr.Yared Fubusa alizaliwa katika Kijiji cha Kiganza, Kata ya Mwandiga, Kigoma Kaskazini,
elimu ya msingi alipatia Kiganza na sekondari aliipatia Mwandiga mwaka 1991-1993 huku kidato
cha tano na sita aliipatia Milambo, Tabora mwaka 1996.

Fubusa ana digrii tatu ya kwanza ikiwa niya Uchumi (Bachelor Degree) aliyoipata mwaka 2000, ya pili ni ya Uchumi na Maliasili (Master Degree) mwaka 2003 na ya tatu ikiwa ni PHD ya uchumi na Maliasili mwaka 2010 zote akiwa alizipata nchini Marekani.

Mbali na kuwa mkufunzi (Lecturer) mwaka 2003-2004 katika chuo cha Virginia African Studies nchini Marekani pia ni mwakilishi na
mkurugenzi wa Gombe School of Environment and Society (GOSESO), Ujenzi wa Chuo Kikuu Gombe
University of Tanzania (GUTA), pia mmiliki wa Gombe High School (Kidato cha Kwanza hadi Sita).

Akiongea na KAY-STALLION Tz,
Dr.Yared Fubusa alitoa sababu za yeye kuamua kugombea Ubunge katika Jimbo hilo na kutoa mipango yake baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge.

Fubusa alisema, anaamua kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini baada ya kuona
kila mbunge anaepita hashughulikii changamoto za wananchi na kutumia Jimbo hilo kama daraja la
kuwapeleka Bungeni na kujinufaisha wenyewe.

Alisema kuwa, wananchi wa Jimbo hilo walikuwa wakitafuta Mbunge ambaye atawatatulia matatizo
yao kwa muda mrefu, na baada ya kuona Mbunge aliyekuwa akiliwakili jimbo hilo kuanzia mwaka
1990 hadi 2005 Harimeshi Kahena hajafanikiwa kuwasaidia waliamua kumpa nafasi hiyo Zitto Kabwe mwaka 2005.

“Wananchi walimpa Zitto dhamana ya kuwawakilisha baada ya kuona sera zake zinalenga kuwatatulia changamoto zao sambamba na ahadi nyingi alizowaahidi” alisema Fubusa.

Aidha Fubusa alisema, baada ya Zitto kuingia Bungeni haikuwa kama wananchi walivyotarajia kwani hakufanya kama sera zake zilivyokuwa zikisema kabla ya kuchaguliwa na mpaka sasa bado changamoto za wananchi ziko palepale.

“Mimi ni mkazi na mzaliwa wa jimbo hili hivyo changamoto zote na namna viongozi wanavyowakilisha jimbo nafahamu, Leo ni miaka
kumi baada ya Zitto kuchaguliwa ila bado kero za wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini hazijatatuliwa licha ya wananchi kuwa na imani na
Zitto kipindi cha kampeni” alisema Fubusa.

Aliongeza kuwa, baadhi ya vijiji katika Jimbo hilo havina Shule, Zahanati pia hata barabara hazipitiki, kitu kinachosababisha wananchi kuhangaika kupata huduma za kijamii kama elimu kwa watoto na matibabu kwa wagonjwa.

Hata hivyo Fubusa alisema kuwa, maeneo ya Manyovu Kanda ya juu ya Jimbo hilo wananchi hulima zaidi kahawa na wananchi hao wamekuwa na Kero kubwa ya muda mrefu kuhusu uuzaji wa kahawa hizo jambo ambalo Zitto aliahidi
kulishighulikia kipindi cha kampeni.

“Badala ya Zitto kutatua tatizo la Kahawa ambalo ni kero kubwa kwa wakulima lakini yeye alitumia
upenyo huo kuwakandamiza wakulima na kuwatumia kama SACOS ya kujinufaisha, kitendo
kilichowakela wakuliwa na kuamua kukata miche ya kahawa na kupanda miti ya mbao baada ya
kuona kahawa haina tija kwao na hakuna wakuwasaidia” alisema.

Fubusa alisema kuwa, anaamua kugombea Ubunge baada ya kuona kila Mbunge anayekuja katika
Jimbo hilo hatatui matatizo ya wananchi bali anajinufaisha yeye mwenyewe na familia yake.

Nina mda mrefu niko hapa kwani ni mzawa wa hapa, na mapungufu ya Wabunge yaliyopelekea wananchi kulalamika kila siku nayafahamu sasa nimeamua kuingia Bungeni ili kufanya kile kilicho washinda Wengine.

Kwa mujibu wa Fubusa, anahitaji kuliwakilisha jimbo hilo ili kufikisha kero za wananchi sehemu
husika ili jimbo hilo liwe na madiliko kama yalivyo majimbo mengine na atawaona wananchi kama waajili wake na atawapa kipaumbele kufanyia kazi wanachokisema badala ya kuangalia mambo yake.

Maisha yangu yote ni kutatua changamoto za wananchi na ninaishi katikati ya jimbo tofauti na
Wabunge wengine wanaoishi mbali na wananchi wao na hata nikichaguliwa sitahamia mjini maisha yangu ni hapa hapa kijijini.

Nimekuja kufanya kile alichoshindwa Zitto katika
jimbo hili, Japo alipata umaarufu mkubwa nchini lakini aliwasahau wapiga kura wake na inatambulika kuwa Zitto alifukuzwa CHADEMA yote ni kwasababu ya mapungufu aliyonayo” alisisitiza
Fubusa.

NEWS: CHADEMA YAPATA MBABE WA ZITTO KIGOMA KASKAZINI NEWS: CHADEMA YAPATA MBABE WA ZITTO KIGOMA KASKAZINI Reviewed by Unknown on 03:36 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.