Recent Posts

NEWS: MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WANNE MKOANI KIGOMA.

MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WANNE MKOANI KIGOMA.

Bi. Zuwena Abdul, mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Buzebazeba, Manispaa ya Kigoma Ujiji,
amejifungua watoto mapacha wanne katika hospitari ya mkoa ya Maweni huku awali akiwa ameshajifungua watoto wengine wanne.

Akizungumza na KAY-STALLION TZ hapo jana, Zuwena alisema kuwa, anajisikia faraja kujifungua
mapacha hao bila tatizo lolote, kwani si kawaida kwa mtu kujifungua watoto wengi kwa njia ya
kawaida.

Alisema kuwa, licha ya kujifungua salama lakini changamoto iliyoko mbele yake ni namna ya kuwalea watoto hao kutokana na familia yake kuishi maisha duni na kabla ya watoto hao yeye na mme wake walikuwa na watoto wanne hivyo jumla anawatoto nane sasa.

“Watoto hawa wanahitaji malezi mazuri sasa kulingana na uduni wa maisha nilionao nawaomba
wasamalia wema, serikali na asasi mbali mbali za kijamii, wanisaidia kwa hari na mari ili niweze
kuwatunza watoto wangu vizuri” alisema Zuwena.

Zuwena anaomba msaada huo kutokana na kwamba hana kipato chochote kumudu kuwatunza
watoto wake kwani yeye ni mama wa nyumbani na mume wake Rajabu Mkangwa, anajishughulisha na shughuli ndogo ndogo za uzalishaji.

Aidha Mama mzazi wa Zuwena, Jaqlina Augustino, mkazi wa Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji, alisema
kuwa uzazi wa mwanae wa kujifunga mapacha wanne uliwashitua mno, kwani licha ya familia za pande zote mbili, yaani upande wa Zuwena na ule wa mume wake kuwa na historia ya mapacha
lakini haijawahi kutokea mtu kuzaa mapacha wanne.

“Kwa kweli hicho kitu kilitushangaza sana na pamoja na hayo tunashukuru Mungu sana kuona
ni maajabu kuzaa kawaida wakati wengine mtoto mmoja tu wanafanyiwa upasuaji, lakini yeye Mungu amemtendea miujiza akazaa kwa njia ya kawaida,” alisema mzazi wa Zuwena.

Afisa Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Maweni, Agnesi Nguvumali, alisema kuwa, Zuwena
alijifungua kwa njia ya kawaida mapacha wanne jana majira ya saa kumi na mbili jioni, ambao kati
yao watatu ni wa kiume na mmoja wa kike,ambapo amesema kuwa mtoto wa kwanza amezaliwa akiwa
na uzito wa kilo 1.8, wa pili kilo 2.5, wa tatu 1.7na wa nne kilo 1.7.

“Tunawatunza kwa njia ambayo tunaita Kangaroo, kama ambavyo Kangaroo yule mnyama
anavyotunza mtoto wake kifuani,” alisema Agnesi.

Alisema kuwa aina hiyo ya utunzaji kwa ngozi ya mama na mtoto kugusana, inamsaidia mtoto
kupata uzito mkubwa kwa sababu ya joto la mama tofauti na njia zilizokuwa zikitumiwa hapo mwanzo ikiwemo ya kuvundika.

“Kikubwa tunachoomba yule mama kama alivyosema ni mama wa nyumbani, angeweza kusaidiwa hasa kwenye maziwa ili aweze kutunza hawa watoto wakaweza kukua; kwa yeyote
atakaeguswa aweze kumsaidia huyu mama,” aliongeza afisa muuguzi huyo.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, Fadhili Kibaya, alisema mpaka sasa hali za watoto hao pamoja na mama yao zinaendelea vizuri.

Hata hivyo Zuwena alitoa mawasiliano yake kwa yeyote mwenye kuguswa na ana nia ya kumsaidia awasiliana nae kwa namba 0759 558472, ikiwa ni
sambamba na kumjulia hari ya wanae.

NEWS: MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WANNE MKOANI KIGOMA. NEWS: MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WANNE MKOANI KIGOMA. Reviewed by Unknown on 23:04 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.