Recent Posts

TAARIFA JUU YA HUKUMU YA OSCAR PISTORIOUS

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa kwenda jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
 
Mwanariadha huyo mlemavu amepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka uliopita.
Jaji Thokozile Masipa ametoa hukumu hio na kueleza kuwa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu kuwa hii ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Upande wa mashtaka ulitaka mwanariadha huyo apewe kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatika na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa ndani ya nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake
 
TAARIFA JUU YA HUKUMU YA OSCAR PISTORIOUS TAARIFA JUU YA HUKUMU YA OSCAR PISTORIOUS Reviewed by Unknown on 05:47 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.