Recent Posts

WAFA KWA KULA UNGA WA MUHOGO!!!

Watu wawili wa familia moja katika kijiji cha Miramba mkoani Kagera wamefariki dunia baada ya  kula unga wa mihogo yenye sumu na wengine kadhaa hali zao zikiwa mbaya zaidi katika kijiji hicho
Kamanda wa polisi mkoani kagera Henry Mwaibambe alithibitisha kwa kutokea tukio hilo la kusikitisha, kwamba watu hao walinunua unga wa mihogo na kuula ndipo walipopata tatizo hilo oktoba 20 mwaka huu.
Alisewma kuwa hali za watu hao zilibadilika oktoba 21 mwaka huu saa sita mchana na kukimbizwa hospitali Teule ya Rubya iliyoko Muleba mkoani Kagera.
Katika tatizo hilo waliokufa ni Oliver Wilson[42] ambae ni mama familia hiyo pamoja na mtoto wake Nimilius wilson[5].
Pia kamanda wa polisi aliwataja waliolazwa katika hospital hiyo ni Frorida Wilson[7] na Flora Wilson [7] ambao ni mapacha na Scarion Wilson [2]
Kamanda wa polisi wa mkoani Kagera alisema uchunguzi unaendelea zaidi ili kubaini tatizo hilo la kusikitisha
WAFA KWA KULA UNGA WA MUHOGO!!! WAFA KWA KULA UNGA WA MUHOGO!!! Reviewed by Saidia Turuki on 04:31 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.