Recent Posts

HIKI NDIO CHANZO KIKUBWA CHA SKENDO ZOTE ZA JUSTINE BIEBER KATIKA MWAKA HUU 2014 KUELEKEA MWISHONI.


"Hela zina mchanganya..., dogo ana hela!.., utoto
unamsumbua..." Haya ni baadhi ya Maoni ambayo
# KAY_STALLION tumekuwa tukiyapata kufuatia story
mbali mbali kuhusu skendo za msanii
# Justine_Bieber ambazo tumekuwa tukiziweka juu
yake tangu kuanza kwa mwaka huu.

Ukweli ni huu kuwa lisemwalo lipo kama halipo basi
linakuja na hii pia imetokana na jaridi maarufu la
# Forbes katika chapisho lake jipya linalohusu utajiri
wa mastaa chini ya Umri wa miaka 30
# FORBES_MAGAZINE_30_under_30 ambapo moja
kwa moja unaambiwa kuwa aliye ongoza kwa
mastaa tajili chini ya umri wa miaka 30 ni Justine
Bieber kwa kuwa na utajili wa dola za kimarekani
millioni 80.

Justine Bieber (20) amekuwa ni msanii "Pendwa"
kufuatia nyimbo zake anazoziimba katika miondoko
ya #Pop, lakini moja kati ya wasanii walioandamwa
na vyombo vya habari mwaka huu ni pamoja na yeye
ikiwa ni pamoja na skendo kubwa ya kuandamwa na
majirani zake katika makazi aliyokuwa akiishi huko
# Los_Angels marekani kumtaka ahame kufuatia
vitendo vyake vya fujo, na pia kuna sakata jingine
kubwa alilolipata la kumpa mimba binti aliye
fahamika kwa jina la # Mariah_Yeater ambaye
inadaiwa kuwa alifanya naye mapenzi # Backstage
wakati akisubiri show katika ukumbi wa
# Staples_Center Los-Angels Marekani na baadae
kukataa ujauzito huo.

Licha ya hayo kuna Skendo ya kupiga picha za uchi
na mikanda ya ngono ikiwa ni pamoja na kudhaniwa
kushiriki mapenzi ya jinsia moja na bondia
# Floyd_Mayweather (pichani), yote haya yakichafua
jina lake kutokana na umri mdogo alionao na haya
yote yamekuwa yakisemwa na watu mbali mbali
kuwa kitendo cha #Justine_Bieber kuwa na utajili
mkubwa wakati akingali bwana mdogo ndio tatizo
ambapo pia mke wa raisi wa Marekani,
# Michele_Obama alisha wahi kusema kuwa kama
angekuwa mzazi wake yote hayo yasingetokea kwani
asinge thubutu kumpa Uhuru kiasi hicho.

# Fahamu kuwa kupitia jarida la Forbes la mastaa
tajili chini ya umri wa miaka 30 limemuorodhesha
#Justine_Bieber kama msanii wa kwanza chini ya
umri huo tajili kwa kuwa na utajili wa dola za
kimarekani millioni 80 huku akifuatiwa na hawa hapa:

One Direction – Dola millioni 75
Taylor Swift – Dola millioni 64
Bruno Mars – Dola millioni 60
Rihanna – Dola millioni 48
Miley Cyrus – Dola millioni 36
Jennifer Lawrence – Dola millioni 34
Lady Gaga – Dola millioni 33
Avicii – Dola millioni 28
Skrillex – Dola millioni 18.

HIKI NDIO CHANZO KIKUBWA CHA SKENDO ZOTE ZA JUSTINE BIEBER KATIKA MWAKA HUU 2014 KUELEKEA MWISHONI. HIKI NDIO CHANZO KIKUBWA CHA SKENDO ZOTE
ZA JUSTINE BIEBER KATIKA MWAKA HUU 2014
KUELEKEA MWISHONI.
Reviewed by Unknown on 07:03 Rating: 5

2 comments:

Powered by Blogger.