Recent Posts

SPORTS: MESSI AFUNGUKA KUHUSU HATIMA YAKE BARCA CHELSEA, MAN CITY ZAJIKOKI

>>Mshambuliaji wa FC Barcelona Lione Messi amezungumzia hatima yake ya kuendelea kuchezea Barca baada ya kuulizwa swali wakati akizungumza baada ya kupokea tuzo ya mchezaji wa pili bora wa FIFA hapo jana.

Messi alipoulizwa alizwa kama ataendelea kuchezea katika klabu yake ya Barca au atahamia klabu nyingine itakayo muhitaji alisema hajui kitakachotokea baadae kwani katika maisha ya kawaida hata soka mambo hubadilika.

““I am not sure what’s going to happen, whether I’ll go back to Newell’s. I don’t know where I’ll be next year.” Alisema Messi.

Messi alisema kuwa awali alizunguza kuwa anapenda kumaliza soka lake katika klabu hiyo iliyomkuza lakini anakiri kuwa hakuna anayejua kuhusu kesho itakavyokuwa hasa kwenye dunia ya soka mambo hubadilika kila usiku.


““I always said I’d like to finish my career at Barca and then play at Newell’s but nobody knows what the future holds, especially in the football world where so many things can change overnight.” Alisisitiza Messi.

Kauli hizo za Messi zimekuja siku chache baada ya kutoelewana na kocha wake Luis Enrique ambapo mzozo wao umekuwa ukiendelea kila kukicha.

Messi alikanusha taarifa zilizotolewa kuhusu yeye kuongea na baba yake kuhusu klabu za nchini England ambazo ni Man City na Chelsea ambapo baba yake alimwambia kuwa alizungumza na klabu hizo kuhusu hatima ya mchezaji huyo kama akiondoka Barca.

“ We must be more united than ever. They should not throw sh*t at us. We just want to achieve things for the club.

"It is said that my father spoke with Man City, with Chelsea. It's all lies, it's all lies." Alisema Messi

Messi ameshindwa tena na mpinzani wake wa karibu Mreno Christian Ronaldo katika Tuzo ya Mchezaji bora wa FIFA wa mwaka 2014 ambapo mwaka jana alikuwa wa pili mbele ya Ronaldo.

SPORTS: MESSI AFUNGUKA KUHUSU HATIMA YAKE BARCA CHELSEA, MAN CITY ZAJIKOKI SPORTS: MESSI AFUNGUKA KUHUSU HATIMA YAKE BARCA CHELSEA, MAN CITY ZAJIKOKI Reviewed by Unknown on 22:17 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.