Recent Posts

BURUNDI YAWALILIA WATETEZI WAO WA CHAMA TAWALA BAADA YA KUWAPOTEZA.

Polisi nchini Burundi imesikitika nakutangaza kuwa wanaharakati kutoka chama tawala cha CNDD-FDD wameuawa kwa kupigwa risasi katika mji ulio mashariki mwa nchi ya Gisuru karibu na mpaka wa Tanzania.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wanaume watano waliokuwa wamevaa sare za kijeshi waliingia kwenye eneo moja la burudani jumapili iliyopita ambapo walitumia mbinu kali za kuwafunga wanaharakati hao kabla ya kuwaua.

Aidha katika kutumia mbinu hizo,walienda kwenye ofisi za chama hicho ambapo walifanya uhalifu mwengine wa kuchoma bendera.

Msemaji mkuu wa chama hicho tawala alisema kuwa, waliohusika ni kutoka kwenye kundi lenye siasa kali kutoka upinzani wenye mipango ya kuvuruga uchaguzi ambao utafanyika miezi ijayo mwaka huu.

BURUNDI YAWALILIA WATETEZI WAO WA CHAMA TAWALA BAADA YA KUWAPOTEZA. BURUNDI YAWALILIA WATETEZI WAO WA CHAMA TAWALA BAADA YA KUWAPOTEZA. Reviewed by Saidia Turuki on 07:40 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.