Recent Posts

SPORTS: RONALDO AMPIGA TENA MESSI TUZO YA BALLON D'or 2014


>>Mwanasoka bora wa Dunia mwaka 2013 Mreno Christian Ronaldo amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo tena kwa mwaka 2014 huku akimwa mpinzani wake wa kalibu Lion Messi baada ya kupigwa kura za kumchagua mchezaji bora wa FIFA mwaka 2014 zilizo fanyika nchini Uswisi hivi punde.

Ronaldo alikuwa akichuana vikali na Mshambuliaji wa Barcelona Lion Messi pamoja na kipa wa Ujeruman Manuel Neur ila kutokana na mchango wa Ronaldo katika soka, wadau wa soka wameamua kumchagua yeye kwa mara nyingne.

Aidha Ronaldo alichukua tuzo hiyo mwaka jana iliwa ni tuzo ya FIFA kwa mwaka 2013 na alimshinda tena mpinzani wake Lion Messi, Hivyo Ronaldo amekuwa mchezaji bora wa FIFA wa dunia mara mbili mfululizo ikiwa ni mwaka 2013 na mwaka 2014.

Ronaldo ambaye huchezea klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno amechukua tuzo hiyo kutokana na mchango mkubwa alionao katika klabu yake baada ya kuisaidia kuchukua ubingwa wa ulaya, Copa De Ray, Spanish Super Cup, Uefa Super Cup pia mfungaji bora wa ligi ya Hispain, UEFA na Mfungaji bora wa ligi zote Ulaya.
SPORTS: RONALDO AMPIGA TENA MESSI TUZO YA BALLON D'or 2014 SPORTS: RONALDO AMPIGA TENA MESSI TUZO YA BALLON D'or 2014 Reviewed by Unknown on 21:40 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.