Recent Posts

NEWS: SUDANI KUSINI KUWAONDOA WAFANYAKAZI WA MSF.

SUDANI KUSINI KUWAONDOA WAFANYAKAZI WA MSF.

Shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka la "MSF" limesema kuwa linajiandaa kuwaondoa wafanyakazi wake wa kutoa misaada nchini Sudani Kusini kwa sababu maafisa wa serikali wanatatiza juhudi zao katika eneo hilo linalokabiliwa na mizozo.

Taarifa zilisema kwamba serikali inafanya makusudi kutatiza shughuli za wafanyakazi hao na pia kuwazuia kufikia katika mogimbo ya Darfur na Blue Nile ambako maelfu ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Jeshi la Sudani linakabiliwa na kibarua kigumu kupambana na waasi katika mpaka wa kusini mwa nchi.

Wiki iliyopita shirika la " MSF" lilituhumu jeshi la nchi hiyo kwa kushambulia hospitali katika milima ya Nuba eneo lingine linalozaniwa.

NEWS: SUDANI KUSINI KUWAONDOA WAFANYAKAZI WA MSF. NEWS: SUDANI KUSINI KUWAONDOA WAFANYAKAZI WA MSF. Reviewed by Unknown on 06:21 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.