Recent Posts

HOFU YA TANDA DAR-ES-SALAAM: VIJANA WA PANYA ROAD WAVUNJA AMANI!!.


Katika hali isiyo kuwa ya kawaida ambayo ilipelekea umati wa raia wengi wa Tanzania wanaoishi kona mbali mbali za jiji la Dar-es-salaam kukosa amani huku ikiathiri pia wingi wa wafanyabiashara kulazimika kufunga biashara zao na Wananchi wengine kujifungia majumbani mwao ili kuokoa maisha yao huku taarifa kamili ikiwa ni kuzagaa kwa kikundi cha wezi wanaojiita "Panya Road" ambapo wanasemekana kuvamia
maeneo mbalimbali na kupora vitu, ikiwemo
maeneo ya Sinza, Mwananyamala, Mabibo, Mwenge, Kigogo na Temeke hiyo ikiwa ni pamoja na
kujeruhi watu kwa silaha zao ambazo nyingi ni za jadi yakiwemo Mapanga, Visu, Jambia, Sululu, Bisi bisi, Nyundo na Misumali.

Unaambiwa vijana hao "Panya Road" siku ya jana walikuwa waki randaranda mitaani wakiwa na silaha zao hizo na
kupora mali na kudhuru miili ya Watu kwa kila
watakayekutana naye njiani ambapo tukio hilo lilijiri siku ya jana majira jioni hadi usiku
wa manane huku vijana hao wakitembea katika makundi ya
watu wasiopungua ishirini katika mitaa tajwa ambapo baadhi ya wahanga wa tukio hili walidai kuwa wakikutana
hupora kila kitu hata kudiriki kubaka ikiwa ni pamoja na kupora pia nguo za mwilini.

Kamanda wa Polisi Suleiman Kova siku ya Jana alihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taiga Tbc1 ambapo aliweza kuzungumzia Tukio zima na namna habari zilivyo wafikia na jinsi zilivyo enezwa.

"Sisi kama Jeshi la Polisi tumepata taarifa
vilevile kama walivyopata watu wengine,
kwamba hao vijana maarufu kwa jina la ‘Panya
Road’ walikuwa wamezagaa maeneo mengi, vijana ambao hawana kazi, hawana
maadili mazuri, kwanza kuzungumzis uzito wa
tatizo, jinsi ambavyo habari zilivyovuma
zimevumishwa kubwa zaidi kuliko uzito wa tukio
lenyewe, nataka niwaambie wananchi kwamba
endeleeni na shughuli zenu, hatukatai kwamba hawa vijana wapo.. lakini
nasema suala limekuzwa limetiwa hofu, watu
wamepata hofu kupindukia, wale wanaopeleka uvumi waache kwa sababu
wewe hujaona tukio, ukiletewa message na
wewe unampelekea mtu mwingine hiyo sio
sahihi"
alisema Kova.

Aidha Suleiman Kova aliongezea kuwa Jeshi la polisi lita shughulikia suala la ‘Panya road’ na kuwa
doria itaendelea na aliwasihi wananchi
waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo.

"Haiwezekani panya road wakatawala Dar es
Salaam, haiwezekani panya road wawe na
nguvu kuliko jeshi la Polisi.

Hata hivyo Kova alidai kuwa siku ya jana wali kamatwa vijana wawili muda
mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao.

KAY-STALLION TZ ilipata nafasi ya kuongea na mkazi mmoja wa Tabata ambaye hakupenda jina lake litajwe akitokea tabata karibu na mtaa wa Twiga ambaye alishuhudia tukio hilo la vurugu za 'Panya Road' katika mtaa wa Twiga na kudai kuwa mtaani kwao walilazwa mapema kuanzia saa mbili milango ilifungwa na maduka yote hakuna aliyekuwa akipita nje peke yake isipokuwa wawili watatu ama kikundi.
"Huku Tabata tumelazwa mapema Sana Jana na
hawa panya road, huwezi amini imagine saa mbili kila mtu ndani! na mitaa ya Mandela road ndo kabisaa nasikia huko
wamempiga mtu mapanga hatari!"
alisema mtu huyo.

Pia moja wa stuff wetu Leisha naye alikuwa mmoja wa wahanga wa "Panya Road" ambapo yeye alikutana na sekeseke hilo mitaa ya Ubungo huku akidai watu walikuwa wakikmbia kwa hofu kila mtu akiulizwa utasikia "Paaaanyaa Rooodii haaao".

"Ubungo naenda home navuka pale mataa nikapande gari duuuh palichafuka vby kdg nigong n boda boda but alie kuwa nyuma Yang ndo amegongwa"
alinoambia Leisha muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo za kuzagaa kwa vijana wa 'Panya Road'.

HOFU YA TANDA DAR-ES-SALAAM: VIJANA WA PANYA ROAD WAVUNJA AMANI!!. HOFU YA TANDA DAR-ES-SALAAM: VIJANA WA PANYA ROAD WAVUNJA AMANI!!. Reviewed by Saidia Turuki on 01:47 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.