STAA wa Muziki Nchini Nigeria amefanikiwa ku saini Mkataba mkubwa na kampuni ya Sony Music (Sony DMG) ikiwa ni dili la Dola Millioni Moja na tayari atakuwa rasmi kikazi na kampuni hiyo.
Davido pamoja na Sean Watson, ambaye ni Managing Director wa kampuni ya Sony Music Entertainment waliweza kusign mkataba huo na tayari maneja huyo amedai kazi zitaanza kufanyika na pia ameweza kukisifu kipaji cha Davido “Davido ni msanii mpya kusainiwa na Sony Music Entertainment Africa na tumefurahia kungana naye kwenye kazi na tutahakikisha tunafanikisha malengo yake kwneye muziki.” alisema Watson.
Davido pia kwa furaha kubwa aliweza kushare kile kilicho jiri katika maongezi na wamiliki wa kampuni hiyo ya Sony Music kwa kuweka post yenye mashiko kwa kuandika kuwa Tayari dili limeisha Sainiwa na ndio dili kubwa kwake kama msanii wa kwanza kusaini dili kubwa namna hiyo pia aliweza kugusia namna Mama yake anavyoweza jisikia huko aliko pumzika (R.I.P).
Aidha Adam Granite, Rais wa Sony Music,upande wa Northern & Eastern Europe na Africa kwa ujumla aliweza kusema maneno haya “Tunafuraha ya kumkaribisha Davido kwenye familia ya Sony Music,na tutamtambulisha kama msanii mkubwa kutoka Africa kwa upande wa dunia nzima,na tunafurahi kufanya kazi na Ajiboye meneja wa Davido, pamoja na Efe Ogbeni, atakaye tayarisha album hii kwa niaba yetu“.
DAVIDO ASAINI MKATABA MKUBWA NA KAMPUNI YA SONY MUSIC
Reviewed by Unknown
on
00:12
Rating:
No comments: