James Horner, mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood, ambaye aliandika na
kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni .
Titanic ni filamu iliyompa umaarufu sana na kufahamika ulimwenguni,ila kwa habari ya kusikitisha kwamba amefariki dunia mjini California, kutokana na ajali ya ndege akiwa na
umri wa miaka 61.
James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege,inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali hiyo,na ndege binafsi ndogo ambayo
alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii .
Mwandishi huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali
alitia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu za msanii James Cameron , pamoja na filamu
ya A Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.katika utendaji kazi wake uliotukuka,
James alipewa tuzo ya Oscar kwa filamu ya Titanic na wimbo uliotawala humo na nyinginezo .
James alipewa tuzo ya ushirika katika tuzo ya pili kwenye mashairi na msanii Will Jennings kwa wimbo bora wa asili , na kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika wimbo maarufu wa My Heart
Will Go On, ambao uliimbwa na Celine Dion.
Ajali hiyo ilitokea katika msitu mzito wa taifa la Marekani wa Los Padres, Kaskazini mwa Los Angeles, wakati ndege hiyo ikidondoka ilitoa mshindo mkubwa na kuripuka mara tu ilipotua ardhini.
Ilitoa moto ambao baadaye ulizimwa na kikosi cha wazima moto wa eneo hilo, na kueleza kuwa mashuhuda ambao ni wazima moto.
Msaidizi wa marehemu Horner , Sylvia Patrycja amethibitisha juu ya kifo hicho kwa kuandika kwenye
ukurasa wake wa facebook mwanzoni mwa wiki hii akisema kuwa: "tumempoteza mtu wa kipekee sana ambaye alikuwa na moyo mkuu wa kujitoa na mtu
mwenye kipaji kisicho elezeka.
Aliendelea na kuongeza kuwa amekufa wakati anafanya kitu akipendacho, Asante kwa mchango
wako mkubwa na upendo uliokuwa nao tutaonana mbinguni.
No comments: