Recent Posts

NEWS: JOTO LAUWA WATU PAKISTANI.

JOTO  LAUWA WATU PAKISTANI.

Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa kutokana na idadi
ya watu waliofariki  na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.

Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura "NDMA"  imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.

Jeshi tayari limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka hiyo.

Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.

Maafisa wa afya walisema kuwa vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na
joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.

Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo alisema  kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali ya mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.

Wengine 80 wameripotiwa kufariki katika hospitali
za kibinafsi.

NEWS: JOTO LAUWA WATU PAKISTANI. NEWS: JOTO  LAUWA WATU PAKISTANI. Reviewed by Saidia Turuki on 13:20 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.