Recent Posts

AYEW MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA 8 ENGLAND

Mshambulizi matata wa klabu ya Swansea City Andre Ayew, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita, katika ligi kuu ya Uingereza ya Premier League.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ghana mwenye umri wa miaka 25, amefunga magoli matatu, msimu huku, huku Swansea ikiwa haijapoteza mechi yoyote msimu huu.

Swansea inashikilia nafasi ya nne kwenye msururu wa ligi kuu, ikiwa na alama nane, baada ya kucheza mechi nne

Manchester City ingali kileleni na alama 12 ikifuatwa na Crystal Palace na Leicester zikiwa na alama tisa na nane mtawalia
AYEW MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA 8 ENGLAND AYEW MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA 8 ENGLAND Reviewed by Unknown on 15:12 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.