MAMA mmoja ajulikanae kwa jina la Safi Ramadhani (25) mkazi wa kijiji cha Nkokwa Tarafa ya Buhingu katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili katika Hospitali ya mkoa Maweni.
Akizungumza
na KAY STALLION Hospitalini hapo hii leo, Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa
Kigoma, Dk. Shija Ganai alisema kuwa, mama huyo alifikishwa Hospitalini hapo
jana majira ya saa 11 jioni huku akiwa ni mjamzito baada ya kupewa rufaa kutoka
katika kituo cha afya cha Buhingu.
Picha hii haihusiani na tukio samahani kwa usumbufu mana picha za tukio hazikupatikana |
Alisema
kuwa, awali mama huyo alifikishwa kweye kituo cha afya Buhingu usiku wa juzi,
baada ya kufanya juhudi za kumzalisha mtoto alitoka lakini alitanguliza matako
huku kichwa kikishindikana kutoka hivyo wakaamua kumsafirisha hadi hospitali ya
mkoa.
“Baada
ya kumpokea hapa, wauguzi na madaktali walimpeleka kwenye chumba cha upasuaji
na juhudi za kumtoa mtoto yule zilifanyika lakini ilishindikana huku sababu ya
mtoto kushindwa kutoka ikiwa haijajulikana hivyo ikawabidi kumfanjia upasuaji.
“Kabla
ya kumfanyia upasuaji ilibidi kutenganisha kwanza kichwa na kiwiliwili na baada
ya upasuaji walikuta vichwa viwili ambavyo vilikuwa na viungo vyake vyote kama kawaida baada ya kutenganishwa kwenye
shingo” alifafanua Ganai.
Aidha
Dk. Ganai alisema kuwa, mtoto yule alikuwa ameshafariki mara baada ya harakati
za kumtoa mtoto tumboni kuanzia kituo cha afya cha Buhingu hadi Hospitalini
hapo, ila mama wa mtoto yeye ni mzima japokuwa anauguza majeraha ya zile
purukushani za kumtoa mtoto.
Kwa
upande wake Salum Shaban ambaye ni Mume wa Mama huyo alisema kuwa, mke wake
alipata ujauzito kama kawaida na alikuwa na afya njema muda wote wa ujauzito
ila baada ya kupata uchungu na kufikishwa kituo cha afya cha Buhingu ndipo
mtoto aliposhindwa kutoka na kuwalazimu kupewa rufaa kwenda hospitali ya
Maweni.
“Kilichoshangaza
ni baada ya kufanyiwa upasuaji na mtoto kugundulika ana vichwa viwili, kitu
ambacho hakijawahi kutokea katika uzazi wa mke wangu mana kabla ya ujauzito huu
alishajifungua mara mbili na watoto wote ni wazima hawana matatizo yoyote”
alisema Shabani.
MAMA AJIFUNGUA MTOTO MWENYE VICHWA VIWILI KIGOMA
Reviewed by Unknown
on
05:26
Rating:
No comments: