Klabu
ya Manchester United imethibitishwa kuwa inajaribu kumrejesha mshambuliaji
matata wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ili kuongeza nguvu klabuni hapo.
Kocha
wa Mashetani Wekundu Louis van Gaal amethibitisha kuwa wanawafuatilia wachezaji
kadhaa akiwemo Ronaldo kwa nia ya kuwarejesha Old Trafford ilikuiimarisha
ushindani wake msimu huu.
''Kwa
kiwango kikubwa wengi wa wachezaji tunaowataka hawaachiki, Kumhusu Ronaldo, kwa
hakika tunasubiri thibitisho kwa udi na uvumba'' alisema Van Gaal.
Mshambulizi
huyo machachari aliihama man United katika msimu wa 2009 akielekea Real Madrid kwa
kitita cha pauni milioni 80 na tangu atue Madrid Mreno huyo ameibuka kuwa
mfungaji hodari wa mabao wa klabu hiyo bingwa mara kumi barani ulaya.
Ronaldo
ambaye ametawazwa kuwa mchezaji bingwa wa dunia mara tatu aliweka rekodi ya
kuifunga Real Madrid mabao 323 ambapo rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na
Raul Gonzalez.
Ronaldo
aliwasili Utd akitokea Sporting Lisbon kwa
kitita cha pauni milioni £12.24 pekee
ambapo akiwa Old Trafford Ronaldo alifunga mabao 118 katika mechi 292.
Alipotua
Santiago Bernabéu Ronaldo alishinda taji moja la La Liga ,taji moja la ubingwa
wa bara Ulaya mbali na vikombe kadha vya mashindano ya Uhispania katika kipindi
cha miaka 6.
VAN GAAL APANIA KUMRUDISHA RONALDO MAN U
Reviewed by Unknown
on
03:10
Rating:
No comments: