>>Baada ya kugawana muda wa
kuwa kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini uingereza, hatimaye Vigogo Arsenal na
Manchester city wamesalimu amri na kumpisha Leicester ambay ndiye anaeongoza
mpaka sasa.
Mabadiriko hayo ni baada ya West
Brom kuishangaza Arsenal kwa kuilaza 2-1 wakati Vijana wa Jurgen Klopp, Liverpool
wakiwasambalatisha Man City katika uwanja wao wa Etihad na kuondoka na ushindi
wa 4-1.
Katika mchezo wa Arsenal, Gunners
walikuwa wakwanza kupata bao kupitia Oliver Giroud, lakini baadae Rondon aliisawazishia
West Brom huku bao la kujifunga la Mikel Arteta ziliifanya West Brom kuongoza
kwa mabao 2-1.
ambapo mpaka mpura unaisha West Brom iliondoka
na pointi tatu muhimu na kuiteremsha Arsenal hadi nafasi ya nne.
Licha ya Arsenal kupata penalt, Santi Carzola alipiga nje mkwaju
huo baada ya Sanchez kuchezewa madhabi
ndani ya eneo la hatari na kupoteza nafasi ya kipekee ya Arsenal kusawazisha
mambo n kugawanya alama.
Mpaka mpira unaisha West Brom ilikuwa
mbele kwa mabao 2-1 iliondoka na pointi tatu muhimu na kuiteremsha Arsenal hadi
nafasi ya nne.
Katika uwanja wa Etihad, Liverpool walionyesha
kufufuka baada ya kuonyesha ujasiri dhidi ya matajiri wa Manchester City, Wanasamba,
Firminho na Coutinho walishirikiana kuwatesa mabeki wa City huku kila mmoja
akifunga bao baada ya Erick Mangala kujifunga na Skertel akahitimisha kwa
kufunga bao la nne.
Bao la Kun Aguero halikutosha
kuizuia Liverpool kuondoka na pointi tatu na Ushindi dhidi ya Man City ni
ushindi wa pili kwa Klopp kupata mbele
ya timu kubwa zaidi baada ya kuilaza Chelsea 3-1 wiki chache zilizopita.
Leicester city na Machester United
ndio wanaongoza ligi hiyo kwa alam 28 na 27 wakati hari ikiendelea kuwa mbaya kwa
Aston
villa 5.
Matokeo ya Jumamosi EPL.
Watford 1 - 2 Manchester United
(Vicarage Road)
Chelsea 1 - 0 Norwich City (Stamford
Bridge)
Newcastle United 0 - 3 Leicester
City (St. James' Park)
Swansea City 2 - 2 Bournemouth
(Liberty)
Everton 4 - 0 Aston Villa (Goodson
Park)
West Bromwich Albion 2 - 1 Arsenal
(The Hawthorns)
Southampton 0 - 1 Stoke City (St.
Mary's)
Manchester City 1 - 4 Liverpool
(Etihad )
HAPATOSHI LIGI KUU ENGLAND: LEICESTER YAKAA KILELENI
Reviewed by Unknown
on
14:03
Rating:
No comments: