Recent Posts

ENTERTAINMENT: KAYUMBA JUMA MSHINDI BSS 2015, CHRISTIAN BELLA AWA MILLIONER STEJINI, RUN TOWN WA NIGERIA BURUDANI YAKE YAGEUKA MWANGA WA MSHUMAA!!.

KAYUMBA JUMA MSHINDI BSS 2015, CHRISTIAN BELLA AWA MILLIONER STEJINI, RUN TOWN WA NIGERIA BURUDANI YAKE YAGEUKA MWANGA WA MSHUMAA!!.

Usiku wa kuamkia jana zilikuwa zikifanyika fainali za kumtafuta #Star mpya wa #Bongo_Star_Search_2015, pale KING SOLOMON HALL, Namanga ambapo unambiwa katika mashindano yote yaliyo tokea ya BSS haijawi tokea shindano likasumbua vichwa vya majaji (Salama Jabir, Master-J, na Madam Lita) kama hili la mwaka huu na hii yote ni kutokana na vijana wenye vipaji kuchukua fursa kuonyesha umati wa Watanzania kuwa Tanzania ina vipaji vingi sana vya kuimba.

Fainali hizo zilizo malizika saa 8 usiku ziliumiza vichwa vya majaji hasa katika tano bora ambayo mchujo wake ulifanyika baada ya kila msanii kuimba kwa #Round ya pili na kusababishi upofu kwa majaji nani atoke na nani abaki ambapo mzozo huo ulitokea kutatuliwa na Kura zilizo kuwa zikipigwa na mashabiki waliopo majumbani wakichangamana na waliokuwepo kushuhudia ili kuhakikisha hakiharibiki kitu!.

Kayumba Juma kutoka Temeke Dar-es-Salam ndiye aliye ibuka na ushindi wa kitita cha Tsh.Millioni 50 huku karata yake ya mwisho ya kuimba akiimalizia kwa wimbo wa #Isha_Mashauzi-MAMA na tatu bora yake Mshindi wa Pili akiwa ni Nassib Fonabo na watatu kutoka katika fainali hizo ni Frida Amani wote hawa wawili wakitokea #Arusha.

Kwa upande wa burudani iliyo kuwepo ya wasanii Christian Bella alionekana kukonga nyoyo za watu kwa wimbo wa #Nani_Kama_Mama na kujikuta akimwagiwa Pesa na kutunzwa  Pesa nyingi sana ukiringanisha na wasanii Wengine hivyo kuwapa wakati mgumu Walinzi wake kuokota hela na kupunguza umati wa mashabiki walionyanyuka kumtunza.

Kwa upande wa msanii kutoka Nigeria RunTown anaye tamba na wimbo wa Gallado burudani yake ilikosa ushabiki wakutosha kama ilivyo kuwa kwa wasanii wa Nyumbani kutokana na watu kutozijua nyimbo zake vizuri kwa upande wakuimba kwa kuitikia.

Wasanii wa hapa hapa Nyumbani ambao walitoa burudani ya kutosha ni pamoja na Aika na Nahreel (NAVY-KENZO), Kala Jeremiah, Peter Msechu, Yamoto-Band, na Ben Pal.

#Fahamu washindi wa BSS 2015 tano bora watakuwa katika usimamizi (Management) ya TipTop Conection kwajili ya kutoa kazi zao za muziki  pamoja na Kolabo ya wote.

ENTERTAINMENT: KAYUMBA JUMA MSHINDI BSS 2015, CHRISTIAN BELLA AWA MILLIONER STEJINI, RUN TOWN WA NIGERIA BURUDANI YAKE YAGEUKA MWANGA WA MSHUMAA!!. ENTERTAINMENT: KAYUMBA JUMA MSHINDI BSS 2015, CHRISTIAN BELLA AWA MILLIONER STEJINI, RUN TOWN WA NIGERIA BURUDANI YAKE YAGEUKA MWANGA WA MSHUMAA!!.
Reviewed by Unknown on 07:39 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.