Recent Posts

BARAZA LA SANAA (BASATA) LIMEUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO.

Baraza la Sanaa Tanzania 'BASATA' lilimpa onyo kali Msanii Nay wa Mitego kwa kumwagiza kuacha kuutangaza wimbo wake wa 'Shika Adabu Yako' katika media, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Hata hivyo BASATA haikuchukua muda kutangaza kuufungia wimbo huo na kudai kuwa pamoja na hayo wasanii wengi wanatumia muda mwingi kubuni na kutengeneza kazi nzuri, lakini kuna wachache ambao wanaharibu, hivyo kama wasimamizi wa sanaa hawata wafumbia macho watu hao.

“Wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri, kwa kubuni kazi zenye ubora na zinazolipa sifa taifa, wachache wanaharibu, wanapakaa matope , BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache wanaotaka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni, wasio na staha,wa kudharaulika”, ili andika BASATA katika ukurasa wake wa Twitter. j

#FAHAMU: Nay wa Mitego kupitia wimbo wake huu hivi sasa yupo katika Bifu na Ommy Dimpoz huku wakirushiana vijembe katika mtandao wa Instagram baada pia ya kumtaja katika wimbo wake kuwa eti! "Huyu jamaa anajiita Dimpoz, Poz kwa Poz
Wanae wanalalamika hawamjui shemeji
Kitaani kuna tetesi mwana hapigi mechi
Mara oh jogoo hawiki, huwa haonyeshi shemeji"
BARAZA LA SANAA (BASATA) LIMEUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO. BARAZA LA SANAA (BASATA) LIMEUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO. Reviewed by Unknown on 01:51 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.