Recent Posts

MANENO YA NICK MINAJ BAADA YA HUKUMU YA MEEK MILL: "I WILL SUPPORT MEEK TO STAY OUT OV TROUBLE"

Baada ya kukutwa na Hatia ya kutozingatia muda uliyotolewa na Mahakama kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini Marekani  dhidi ya vitendo vya matumizi ya Silaha bila kibali maalum na Madawa ya Kulevya Rappa kiungo wa kundi la MAYBACH MUSIC GROUP, Meek Mill amehukumiwa kifungo cha nje ya jela cha Siku 90 yaani miezi 3.
 
 Meek Mill amehukumiwa kifungo cha nje ya jela kikiwa na maana atakaa muda wote katika eneo maalum hasa makazi yake kwa muda wa miezi mitatu na pia atavishwa  kifaa cha kuonyesha alipo katika maeneo ya Mguuni (Gps Ankle Blacelet), muda wote wa siku 90 akiwa ndani kwake.
Meek Mill katika  kifungo hicho hataruhusiwa kufanya jambo lolote la kimuziki ikiwemo: kurap, kufanya show au kutoa muziki katika muda huo ambao adhabu itaanza.

Adhabu hii itaanza March 1 2016, ambapo pia Jaji aliye hukumu kesi hii, Genece Brinkley ametoa adhabu nyingine ya muda wa matazamio wa miaka sita tena (Pobation Time) ilikuangalia kama Rapa huyo ni mtiifu wa Sheria dhidi ya Matumizi ya Silaha kinyume cha Sheria na Matumizi ya Dawa za Kulevya.



Nicki Minaj alikuwa pembeni mwa mpenzi wake Meek Mill wakati rapa huyo anasomewa hukumu yake ya kuvunja masharti ya kifungo cha nje, ambapo katika kumuhakikishia Jaji na mashabiki wa Meek Mill aliweza kusema kuwa atamsaidia Meek Mill kufuata masharti ya mahakama kama alivyotajiwa na jaji.

FAHAMU: Meek Mill amekuwa kwenye muda wa matazamio yaani  probation toka mwaka 2009 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya na silaha kinyume cha sheria.
MANENO YA NICK MINAJ BAADA YA HUKUMU YA MEEK MILL: "I WILL SUPPORT MEEK TO STAY OUT OV TROUBLE" MANENO YA NICK MINAJ BAADA YA HUKUMU YA MEEK MILL: "I WILL SUPPORT MEEK TO STAY OUT OV TROUBLE" Reviewed by Unknown on 00:06 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.