IMEKUWA ikiaminika kuwa kwa wasanii ambao ni ndugu ni ngumu kutengana mfano: Kama Joh Makini na Niki wa Pili ambao hivi sasa wanafanya vizuri kupitia muunganiko wao katika kundi la Weusi, lakini hali ya kiutofauti imeweza kulikumba kundi la wana ndugu Peter and Paul Okoye wa P square ambao walikuwa wana ugomvi kuhusu kusimamiwa na Kaka yao Mkubwa Jude Okeye ambapo kulikuwa kuna pingamizi kati yao mmoja akitaka waendelee kusimamiwa na kaka yao na mwingine akipinga.
Peter Okoye wa P Square ametoa maelezo kamili kwa mashabiki wa P Square kuhusu ushirikiano wao kwenye muziki wa kundi hilo na kusema vitu vitatu muhimu ambavyo ni mashabiki wanaweza kutoa ushirikiano wao ni kumpa nguvu Paul Okoye kama Rudeboy , Peter Okoye kama Mr P na kwa wote wawili kama P Square bila kubagua.
Paul Okoye ana record lebel iliyopewa jina RudeBoy Records na ana wasanii Muno na Lucy huku Peter Okoye anayetumia Mr P anafanya kazi na meneja mpya Olatunde Michael na atakuwa akifanya show zake mwenyewe.
HUENDA HUU UKAWA MWISHO MBAYA WA PSQUARE BAADA YA MANENO HAYA YA PETER.
Reviewed by Unknown
on
03:05
Rating:
No comments: