Recent Posts

BENTEKE AIPAISHA LIVERPOOL IKIIUA BOURNEMOUTH

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi klabu ya Bournemouth ikiwa ni mchezo wake wa pili katika ligi kuu nchini England.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja Anfield, bao pekee la ushindi la majogoo wa hao liliwekwa kimiani na mshambuliaji mpya wa timu hiyo Mbelgiji Christian Benteke katika dakika ya 26 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Jordan Henderson.

Kwa ushindi huu timu hiyo inasogea mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 6 na mabao mawili.

Huku Bournemouth wakisalia nafasi ya 19 wakiwa hawana alama hata moja baada ya kucheza michezo miwili ya ligi.

Kwa upande wake Meneja wa klabu ya Bournemouth ya nchini Uingereza,Eddie Howe amelalamikia maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo na kusema kuwa maamuzi yaliyofanywa ni kinyume na matarajio ya wengi katika mchezo waliopoteza dhidi ya Liverpool na  hayasameheki.

Utata wa bao la Christian Benteke lulikuja baada ya Benteke kufunga goli kufuatia  kupata kross safi kutoka kwa Jordan Henderson ambayo kabla ya hapo Philippe Coutinho alikwisha otea licha ya kutougusa mpira.

Mapema mchezaji wa Bournemouth Tommy Elphick alikaribia kufunga lakini alinyimwa kwa kucheza vibaya.''Huwezi kupingana na maamuzi na mambo hayo yalitunyima alama muhimu'' alisema meneja wa Bournemouth mwenye miaka 37 Eddie Howe.

Howe alisema kuwa atajaribu kutizama nini kitafuatia kwa mwamuzi wa mchezo huo Craig Pawson pamoja na waaamuzi wasaidizi.
BENTEKE AIPAISHA LIVERPOOL IKIIUA BOURNEMOUTH BENTEKE AIPAISHA LIVERPOOL IKIIUA  BOURNEMOUTH Reviewed by Unknown on 11:32 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.