Recent Posts

NEWS: PROFESA LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF.

PROFESA LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF, Profesa Ibrahim Lupumba amejiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho kwa madai kuwa UKAWA wameshindwa kusimamia makubaliano waliyokuwa wameyafikia, hivyo yeye atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CUF

Hizi ni baadhi ya Kauli za Prof. Lipumba akiwa na waandishi wa habari

'Nawaomba radhi sana Wanachama na Wananchi walioniamini na kuonesha mapenzi makubwa ktk Uongozi wangu'

'Najua hili litawashtusha, litawakasirisha, litawafadhaisha. Ndani ya Chama mimi naonekana ni kikwazo'

Naonekana siwezi kuwa na mchango kama Kiongozi ktk Mapambano ya kudai haki sawa'

Nimeona niachie ngazi lakini niendelee kushiriki shughuli nyingine zinazohusu Maendeleo ya Chama Kiuchumi'

'Ninaendelea kuwa Mwanachama wa CUF na nimelipia Kadi ya Uanachama mpaka 2020, sina mpango wa Kujiunga ACT'

Taarifa ya kung'atuka niliitoa August 01 2015, nilisubiri kukamilisha masuala ya UKAWA ndio nitoke'

'Naubariki Umoja wa UKAWA ili tusimamie kupata Katiba iliyopendekezwa na Wananchi'

'Ni kweli nilishiriki kumkaribisha Lowassa UKAWA lakini dhamira na nafsi yangu inanisuta'- 

'Tumekaribisha watu wa CCM ambao waliipinga Rasimu ya Katiba, najiuliza tutaweza kusimamia malengo ya UKAWA'

'Nimeona nijikite kwenye kufanya Utafiti wa Ushauri wa masuala ya Uchumi ili kuinua Uchumi wa nchi'

Sijashawishiwa na mtu yoyote kuachia ngazi,ni dhamira na nafsi yangu.. asisingiziwe mtu kwamba amenishauri'

'CUF bado imo ndani ya UKAWA, nitashiriki Kampeni za Uchaguzi kama mwanachama wa kawaida wa CUF'

NEWS: PROFESA LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF. NEWS: PROFESA LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF. Reviewed by Unknown on 22:44 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.