Hatimaye beki kisiki wa klabu ya soka ya Real Madrid Sergio Ramos, amesaini mkataba mpya na timu yake baada ya kuhusishwa na kuihama timu hiyo na kutimuikia katika klabu ya Manchester United iliyokuwa ikimuhitaji kwa udi na uvumba.
Mlinzi huyu alikua anahusishwa kujiunga na miamba wa soka wa England klabu ya Manchester United kama sehemu ya mabadilishano na kipa anayewindwa na Real David De Gea.
Baada ya kusaini mkataba huo Ramos amesema “ Mawazo yangu ni kuwa hapa na kustaafu soka nikiwa hapa kama raisi wa timu ataruhusu,nashukuru nina changamoto mpya nikiwa nahodha wa timu” .
RAMOS KUSALIA REAL MADRID BAADA YA KUSAINI MIAKA MITANO
Reviewed by Unknown
on
10:34
Rating:
No comments: