ENTERTAINMENT NEWS: LATIFFAH NASEEB ABDUL A.K.A TIFFAH DANGOTE A.K.A PRINCESS TIFFAH NDIO JINA LA MTOTO WA DIAMOND AMBAYE AMEKUWA MAARUFU KWA MASAA KADHAA BAADA YA KUZALIWA!. NA HUENDA NI AFRIKA NZIMA! KUTOKANA NA UMAARUFU WA DIAMOND!!.
LATIFFAH NASEEB ABDUL A.K.A TIFFAH DANGOTE A.K.A PRINCESS TIFFAH NDIO JINA LA MTOTO WA DIAMOND AMBAYE AMEKUWA MAARUFU KWA MASAA KADHAA BAADA YA KUZALIWA!. NA HUENDA NI AFRIKA NZIMA! KUTOKANA NA UMAARUFU WA DIAMOND!!.
Siku zote jambo lolote Jema ama baya huwa halijulikani ni muda gani litatokea kutokana na ratiba ya Mwenyezi Mungu kutofautiana kwa
kiwango kikubwa na sisi wanadamu, na hiyo huwa tunaibaini kwa mambo mbali mbali ambayo tunakuwa hatuyajui mfano: Diamond hakujua
kama atakuja kuzaa na Mama tajiri sana kwa upande wa Afrika mashariki pia mtoto wao kuwa
maarufu zaidi hata ya watoto wa Mwanzo wa Zarinah a.k.a the boss lady na mapya mengi ambayo me na wewe hatuyajui.
Mapema jana majira ya ,saa 10 na dakika 40 alfajiri Zari alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike ambaye kwa upande wa Msanii wetu maarufu imekuwa Shangwe sana kupokea baraka ya uzao
wake wa kwanza kutokana na kusubiri kwa hamu kuweza kuitwa baba flani huku katika kulionyesha
hilo Platnum kupitia Instagram aliweka picha ya Mkewe Zari na Mama yake (Mama Diamond) na
kuweka maneno ambayo yametosha kueleza ni furaha gani aliyo nayo ya kupata Mwanae huyo
ambapo aliandika hivi: "Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah.
Taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu na Diamond zimeeleza kuwa Hospitali aliyo jifungulia Zari
haijatwa kutokana na kudai kujali usalama wa Mama na Mtoto licha ya Diamond kudai kuwa
Zarinah amejifungulia nyumbani hapa hapa Tanzania.
Unaambiwa tayari mtoto huyo amefunguliwa account ya
Instagram iliyopewa jina la #princess_tiffah na mpaka sasa ina zaidi ya watu Elfu 40 Huku
kwenye Biography ikiwa na Maneno yanosomeka hivi:
“Welcome to the Next Most Famous Daughter in Africa… My dad and Mom decided to call me Latiffah but I wanna be called Latty or Tiffah.
Zaidi ya yote katika hili Hongera zifike kwa Mr & Mrs Diamond Platnumz kwa kupokea mtoto wa
Kike na Mwenyezi Mungu awawezeshe kumlea katika malezi bora na yanayo zingatia tamaduni
zetu za Afrika daima Amani na Upendo udumu katika familia hii Changa!. Amen!
No comments: