Pichani: Sehemu ya mbeli ya meli hiyo iliyo baki haija zama. |
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa baharini
imekwamisha shughuli na juhudi za utafutaji na uokoaji wa watu takribani mia tatu baada
ya meli ya abiria kuzama katika pwani ya Korea Kusini ambapo mpaka hivi sasa Watu tisa wamethibitishwa kufariki dunia katika mkasa huo.
Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani Heidi C. Agle ameshiriki katika operesheni ya uokoaji huo ambapo ameiambia #BBC kuwa maandalizi yanayo fanyika sasa hivi ni kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho na wakati huohuo Rais Park Geun-hye, amewataka waokozi kuharakisha juhudi zao za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Pichani:Baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu, wakifanya maombi. |
Wapiga mbizi wamekuwa wakikabiliana na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho kilichozama majini siku ya jana.
Taarifa kamili za kuzama meli hiyo zinasema kuwa meli hiyo ilipoteza mwelekeo ikiwa katika safari hiyo ya maji na kufikia hadi hivi sasa baadhi ya familia za waathriwa zimechachamaa kuhoji mwenendo wa nahodha aliyekuwa akiendesha meli hiyo, hata hivyo nahodha wa meli hiyo Lee Joon-seok aliomba msamaha kwa kusema ana majuto mengi na hajui hata la kusema.
Mpaka sasa watu walio fariki idadi yao inafika Tisa ambapo miongoni mwa wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa miaka 17 na mwaliamu wao mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi mmoja wa meli hiyo nawengine wliofariki bado hawajatambuliwa huku Takwimu za idadi ya watu katika meli hiyo zinasema kuwa watu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287 wakiwa bado hawajapatikana hadi hivi sasa.
#Credits:BBC
HALI BADO TATA KATIKA UOKOAJI MELI ILIYOZAMA KOREA.
Reviewed by Unknown
on
03:19
Rating:
No comments: