Recent Posts

KIM KARDASHIAN AWAFICHA DADA ZAKE KUHUSIANA NA ENEO AMBALO NDOA KATI YAKE NA KANYE WEST ITAFANYIKA!!.

Pichani: Kanye West akimcheki Kim Kardashian katika majaribisho ya gauni kwa ajili ya Harusi.
Eneo ambalo ndoa kati ya Kanye West na mchumba wake Kim Kardashian ambae pia ni Mama wa mtoto wake North West linge takiwa kujulikana mapema kabla ya kuanza mwezi kamili wa ndoa yao ambao ni May mwaka huu bado limekuwa gumzo kutokana na wawili hao kuweka usiri kuhusiana na Eneo hilo japo wamekwisha kutaja kuwa ndoa itafanyika jijini Paris Ufaransa lakini bado haija julikana Mtaa wala kitongoji ndoa hiyo itakapo fanyika.

Hali hii imeendelea hivyo hadi kufuatia Kim mwenyewe kuwaficha dada zake pia ambao ni Kourtney, Khole, na Kyle ambao kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa USWEEKLY.COM zinasema kuwa Madada hawa
kwa shauku kubwa walifanya jitihada za juu na chini kama ndugu waweze kujulishwa eneo hilo lakini imekuwa si kitu kufuatia kiapo cha usiri huo kati ya Kanye na Kim kutowatajia watu au mtu yoyote hadi pale walipo dai wao kuwa mpaka tarehe zitakapo sogea na ni wakati wageni waalikwa na wahusika watakapo sogea mjini Paris kwa ajili ya Shughuli hiyo ndipo watakapo weza kutajiwa sehemu husika.

Ni mshangao mkubwa pia kutokana pia na Wageni waalikwa wenyewe kutojua eneo husika kwani tarehe zinazidi kusonga mbele na siku husika imeshatangazwa kuwa ni mwezi May tarehe 24 ndio Kim Kardashian ataongezea jina jingine la ukoo yaani Kim Kardashian West na cheo cha kuitwa Mrs West na upande wa Kanye West kuvaa Ukichwa wa kuongoza familia ambayo imekwisha jaaliwa mtoto mmoja.


KIM KARDASHIAN AWAFICHA DADA ZAKE KUHUSIANA NA ENEO AMBALO NDOA KATI YAKE NA KANYE WEST ITAFANYIKA!!. KIM KARDASHIAN AWAFICHA DADA ZAKE KUHUSIANA NA ENEO AMBALO NDOA KATI YAKE NA KANYE WEST ITAFANYIKA!!. Reviewed by Unknown on 03:03 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.