Vikosi vya usalama nchini Nigeria vinawasaka wasichana mia moja waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Boko Haram katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo la Borno, ambapo Wasichana hao walikuwa wakifanya mitihani yao walipotekwa nyara .
Kwa mujibu wa Taarifa za #BBC zinasema kuwa Utekaji nyara huo umefanyika katika eneo ambalo kundi la Boko Haram linatumia katika kuendesha sana shughuli zake ambapo kuna wasiwasi wasiwasi kuwa huenda wasichana hao wamepelekwa katika eneo la msituni katika jimbo hilo karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon.
Aidha Taarifa zaidi zinasema kuwa lori lililotumika kuwasafirishia wanafunzi hao, lilipatikana likuwa limeegeshwa kando ya barabara.huku taarifa nyingine
zinasema kuwa wapiganaji hao wanafahamu vyema eneo hilo ambalo wamekuwa wakiendeshea harakati zao, na kwamba wanajeshi hawajaweza kuwafurumusha kutoka katika maficho yao msituni
Seneta wa jimbo hilo Ali Ndume, alitoa taarifa kupitia # BBC kuwa lori kubwa lililotumiwa kuwabeba wasichana hao limepatikana na huenda kwa sasa wasichana hao wanatembea kupitia njia ya msituni.
Awali Msichana mmoja aliiambia BBC kuwa yeye na wenzake walifanikiwa kutoroka waliporuka kutoka kwenye lori hilo.
WANAJESHI NIGERIA KUWASAKA WASICHANA WALIOTEKWA.
Reviewed by Unknown
on
06:56
Rating:
No comments: