Recent Posts

WASICHANA WENGINE 14 WAFANIKIWA KUTOROKA KATIKA MIKONO YA WATEKAJI WA KUNDI LA BOKO HARAM.

Pichani: Baadhi ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram
wasichana 14 wengine wamefanikiwa kutoroka katika mikono ya wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Boko Haram waliowatekanyara Jumatatu usiku wa wiki hii.

Kamishna wa elimu katika jimbo la Borno nchini Nigeria Musa Inuwo Kubo amesema kuwa , wasichana 44 hadi hivi sasa wamefanikiwa kuwatoroka watekaji hao na kwamba wasichana wengine 85 hawajulikani walipo kufuatia utekaji nyara huo .
Hata hivyo Vikosi vya Usalama, pamoja na makundi ya vijana wa  usalama mitaani pamoja na familia za wasichana hao waliotekwa nyara zinaendelea kuwatafuta.

Wasichana hao wanaaminika kutekwanyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Boko Haram, ambapo kupitia  #BBC  taarifa kuhusiana na
nchini Nigeria zinasema kuwa kipindi cha nyuma wasichana wamekuwa wakitekwanyara na kundi hilo lakini sio katika kiwango kama cha hivi karibuni
.
Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa wapiganaji hao wamekuwa wakipinga kuwepo kwa elimu ya kidunia na kwamba wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu.
WASICHANA WENGINE 14 WAFANIKIWA KUTOROKA KATIKA MIKONO YA WATEKAJI WA KUNDI LA BOKO HARAM. WASICHANA WENGINE 14 WAFANIKIWA KUTOROKA KATIKA MIKONO YA WATEKAJI WA KUNDI LA BOKO HARAM. Reviewed by Unknown on 02:07 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.