Recent Posts

JE WEWE NI MPENZI WA FILAMU?!.


UNAMJUA VIPI JASON-STATHAM?!!

Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Bacon kutoka katika filamu ya Lock, pia kama Jake Green kutoka katika filamu ya hivi karibuni ya #Revolver, pia na jina la Turkish kutoka katika filamu ya Snatch, lakini moja kati ya yote ni Frank Martin alilotumia kwenye filamu ya #TRANSPORTER1_2_3.

Pia Statham amepata kuonekana katika filmu nyingi sana za Kimarekani, Filamu hizo ni kama vile The Italian Job, Crank, The One ya Jet Lee na War ambazo hizi mbili alicheza na miwgizaji filamu mashuhuri wa Kichina Jet Li, vilevile katika The Transporter, humo alicheza kama nyota kiongozi wa filamu hiyo na inaamika kwamba ile ndiyo iliyomfanya aonekane zaidi na kujipatia soko kwa watu wa Marekani na kwingineko Duniani.

Statham alizaliwa mjini Shirebrook, Derbyshire Uingereza septemba 12-1972 na baadaye kuhamia mjini London, Ni mtoto wa pili wa wazazi ambao mmoja wao alikuwa mwimbaji na mwingine designer wa nguo na chimbuko lake la kipaji chake lilitokana na kukulia katika maisha ya kimichezo na ni mwogeleaji mzuri na mwanariadha kwani kama ulisha wahi kuona filamu yake ya #CRANK utakuwa umenipata vilivyo, lakini richa ya hivyo amewahi kushinda mashindano ya kimataifa ya mbio kwa mwaka wa 1992, Vilevile amewahi kuwa mwanachama wa Kikosi cha Waogeleaji cha Taifa cha Britain kwa takriban miaka kumi na miwili, Pia Statham ni mtaalam wa martial arts na Kick Boxing na huko ndiko palipo chimbua kipaji chake cha uigizaji na kuingia rasmi katika filamu za #Action na ndizo nyingi alizo wahi kucheza lakini pia ifahamike kuwa kama alivyokua marehemu #Paul_Walker katika kuchezea magari basi hata Statham ni mtaalamu pia kwani kama ulisha wahi kuona filamu zake hasa Transporter(1,2,3), Death race, Italian-Job, pia na Fast and Furious 7 ambayo itatoka mwaka kesho zote hizi zinampa wadhifa mzuri katika kuendesha magari na kuonesha kiasi gani alivyo mbunifu katika kazi zake za uigizaji.

FILAMU ALIZOWAHI KUCHEZA NA BADO ZIPO KWENYE CHATI NI KAMA:

*Ghost of Mars.
*The One.
*Mean Machine.
*Handsome Rob.
*Transporter 1,2,3.
*Revolver.
*Crank.
*Chaos.
*The pink Panther.
*War.
*In the name of the King.
*The bank Job.
*Death Race.
*Italian Job.
*Expendable.
Na nyinginezo nyingi!.
JE WEWE NI MPENZI WA FILAMU?!. JE WEWE NI MPENZI WA FILAMU?!. Reviewed by Unknown on 07:04 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.