Recent Posts

UP COMING HITS!.



50 CENT KUFANYA KOLLABO NA DRAKE PAMOJA NA RIHANNA.
Kutokana na kufanikiwa kwa Rappa na Bosi wa kundi la #G_unit Curtis James Jackson III "50 cent" kupitia muziki lakini wiki iliyopita kupitia kipindi cha #SiriusXM's_Shade cha Mtv aliweza kufunguka vilivyo kuhusiana na kazi zake na kueleza mipango yake ya ziada katika kazi yake ya muziki na pia kugusia kuhusiana na watu ambao amep...anga kufanya nao kollabo.

Fifty kupitia kipindi hicho kilicho rushwa saa 2:00usiku wa jumatatu ya wiki iliyopita aliweza kufunguka kwa kusema wasanii wanaofanya kitu kimuziki ambacho yeye binafsi hawezi kukifanya hao hufanya kitu cha tofauti na ndio anaotaka kufanya nao kazi ambapo aligusia kuhusiana na mpango wa kufanya kazi pamoja na Drake na Rihanna.

"Imenibidi kuweka mikakati ya kufanya nyimbo ya pamoja ambayo nitamshirikisha Drake na Rihanna kutokana nataka kufanya dili la utofauti katika muziki hususani kwenye mambo ya kollabo, ambapo binafsi nikimzungumzia Rihanna ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanaoweza kuimba #Solo nzuri! kwani kwa kipindi cha nyuma pia nilisha wahi kufanya kazi na Beyoncé tukaimba nyimbo inayoitwa 'Thug Love' mnamo miaka ya 98 lakini kutokana na mambo binafsi sikutaka kumtumia tena Beyoncé na ndio nikapata wazo la kufanya kazi na Rihanna, Kuhusiana na Drake daah! sidhani kama kuna msanii anaeweza kumpiku Drake kwa staili yake ya uimbaji", alisema 50 cent.

Hivi karibuni Fifty ameandaa tamasha lake binafsi linalojulikana kama #LP_Animal_Ambition ndilo lililo mjengea ukaribu zaidi kati yake na kina Drake na Rihanna ambapo tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 3 ya mwezi Juni na kutakuwa na wasanii waalikwa ambao 50 aliwataja kuwa ni pamoja na: Trey songz, Jadakiss, Styles P na Yo Gotti na pia kuhusiana na dili hilo la kollabo ya Drake na Rihanna limesha tiki na wameanza kazi rasmi na kuwataka ma #Fans wao wasubiri kupokea kazi hizo.
UP COMING HITS!. UP COMING HITS!. Reviewed by Unknown on 07:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.