Recent Posts

AL AHLY MWENDO MPETO!!.


MAFARAO AL AHLY YANUSA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

<>TIMU ya Al Ahly ya Misri imebisha hodi hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Difaa El- Jadidi ya Moroco Uwanja wa Jeshi la Anga mjini Cairo Misri jana.

Shukrani kwake Abdallah Said aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20 na sasa Al Ahly iliyovuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika itahitaji sare katika mchezo wa marudiano kutinga hatua ya makundi.

Katika mechi nyingine za jana, AS Real iliifunga 2-1 Djoliba FC zote za Mali, AC Leopards ya Kongo iliifunga 2-0 Medeama ya Ghana, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ilifungwa 2-1 nyumbani na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Coton Sport ya Cameroon ilishinda 2-1 dhidi ya Petro Atletico ya Angola.


AL AHLY MWENDO MPETO!!. AL AHLY MWENDO MPETO!!. Reviewed by Unknown on 07:48 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.