Recent Posts

NEWS: HOFU YA MAGONJWA YA MLIPUKO YATANDA KAGUNGA-KIGOMA

HOFU YA MAGONJWA YA MLIPUKO YATANDA KAGUNGA-KIGOMA.

>>WAKAZI wa Kijiji cha Kagunga kilichopo Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma katika mpaka wa Tanzania na Burundi, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kufuatia maelfu ya raia kutoka Burundi kuzidi kufurika kijijini hapo huku kukiwa hakuna huduma za msingi za kijamii na kupelekea maeneo mengi kuzagaa uchafu.

Zaidi ya watu elfu 20 raia kutoka Burundi ambao wanakimbia machafuko ya kisiasa nchini mwao
kuja kuomba hifadhi nchini Tanzania, wako katika Kitongoji cha Rusolo, kijiji cha Kagunga wakisubiri
kuvuka Ziwa Tanganyika mpaka ng’ambo ya pili upande wa Tanzania kabla ya kusafirishwa mpaka
kwenye kambi ya Nyarugusu.

Kufuatia ongezeko la watu kila siku hali ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile vyoo na huduma za Zahanati maji na chakula ni mbaya sana kulinganisha na idadi ya watu waliopo katika eneo hilo kutokana na Zaidi ya watu 2,000 kuwasili kutoka nchini Burundi na kuweka kambi hapo.

KAY-STALLION TZ imebaini kuwepo kwa Zahanati moja kijijini hapo ambayo ina muuguzi mmoja, pia
baadhi ya sehemu katika eneo hilo zimeanza kutapakaa kinyesi cha binadamu na uchafu mwingine unaotokana na maisha ya kila siku ya watu hao ikiwemo mabaki ya chakula.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rusolo, James Daniel Rusana Tayari vifo vya watu
watatu vimeripotiwa katika eneo hilo na haijafahamika mara moja sababu za vifo hivyo lakini hilo limeibua hofu ya magonjwa ya mlipuko kutokea kijijini hapo.

Kwa upande wake Afisa Usalama Mshiriki wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Ofisi ndogo ya Kasulu, Michael Kiimbila, alisema kuwa mipango inafanywa ili watu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, wafike Kagunga kwa ajili msaada wa huduma za kibinadamu ili kuepusha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Rusolo, walisema tangu mwaka 1972, hawajawahi kushuhudia idadi kubwa ya raia kutoka Burundi kuweka kambi eneo hilo ambapo walizitaka mamlaka zinazohusika
kuchukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo.

Meli ya M.V. Liemba ambayo ilikodiwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kwa ajili ya kusomba raia hao wa Burundi kutoka Kagunga mpaka Bandari ya Kigoma, imeanza
kuelemewa kutokana na wingi wa raia wanaoingia kila siku.

Meri ya M.V.Liemba, ambayo ni kongwe balani Afirika ina uwezo wa kubeba abiria 600 kwa wakati mmoja hivyo kushindwa kukabiliana na wingi wa watu na mpaka sasa Juhudi zinafanywa na Serikali
kwa kushirikiana na maafisa kutoka UNHCR, ili Meli ya M.V.Mwongozo iweze kusaidia kuwavusha raia
hao toka Burundi.

Kwa mujibi wa Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser, alisema waomba hifadhi
walioandikishwa na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma mpaka kufikia Alhamisi walikuwa zaidi ya 6,000, huku zoezi la uandikishaji likiendelea huku idadi ya wanaoingia Tanzania ikiongezeka.

NEWS: HOFU YA MAGONJWA YA MLIPUKO YATANDA KAGUNGA-KIGOMA NEWS: HOFU YA MAGONJWA YA MLIPUKO YATANDA KAGUNGA-KIGOMA Reviewed by Unknown on 15:04 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.