LIGI KUU NCHINI ENGLAND KUENDELEA KESHO.
>>Ligi ya England itaendelea tena wikiendi hii kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto katika siku ya
jumamosi.
Southampton walioko katika nafasi ya 7 huku wakiwa wamejikusanyia alama 57 watakua wenyeji
wa Aston Villa mchezo utakao fanyika katika uwanja wa St Mary's.
Burnley ambao tayari wameshuka daraja watakua katika uwanja wao wa nyumbani Turf Moor
kuwakabili Stoke City.
Katika dimba la Loftus Road QPR watakua na kibarua cha kuwakabili Newcastle huku QPR wakikamilisha ratiba baada ya kuwa wamesha shuka daraja tayari.
Sunderland atakua nyumbani Brittania kuwaalika Leicester City huku kila timu ikihitaji alama tatu
kuweza kujinasua na janga la kushuka daraja.
Tottenham ambao wamepoteza nafasi ya kucheza michuno klabu bigwa ulaya watakua wanasaka
tiketi ya kucheza Europa Ligi watakapo wakabili Hull City.
West Ham walioko nafasi ya 10 watakua katika dimba lao la Upton Park, kupepetana na Everton, Huku Majogoo wa jiji Liverpool waki wakabili Tai wa Crystal Palace.
Ligi hii itaendelea tena jumapili kwa michezo miwili kwa Swansea kucheza Man City huku Manchester United wakionyeshana ubavu na
Arsenal.
No comments: