NORWICH CITY WARUDI TENA LIGI KUU ENGLAND.
>>Klabu ya Norwich City iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza nchini England maalufu kama Championship imefanikiwa kupanda daraja na itashiriki ligi kuu msimu ujao baada ya kushuka daraja msimu mmoja uliopita.
Norwich ilifanikiwa kupanda daraja baada ya kuifunga timu ya
Middlesbrough mabao 2-0 katika mchezo wa mtoano wa kugombania kushika nafasi ya tatu ya
msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini humo ili kupata nafasi ya kupanda daraja ambapo timu
iliyoshika nafasi ya kwanza nay a pili hupanda daraja moja kwa moja.
Huku nafasi ya tatu hadi ya tano zikicheza michezo ya mtoano ili kugombania nafasi moja ya
kupanda daraja na kutimiza timu tatu.
Norwich inaungana na timu ya Bournemouth na Watford ambazo zilikata tiketi ya kushiriki ligi kuu
nchini England mapema.
Msimamo ulivyo baada ya Ligi daraja la kwanza kumalizika nchini England.
1 Bournemouth
2 Watford
3 Norwich
4 Middlesbrough
5 Brentford
6 Ipswich
7 Wolves
8 Derby
9 Blackburn
10 Birmingham
11 Cardiff
12 Charlton
13 Sheff Wed
14 Nottm Forest
15 Leeds
16 Huddersfield
17 Fulham
18 Bolton
19 Reading
20 Brighton
21 Rotherham
22 Millwall
23 Wigan
24 Blackpool.
No comments: