Ronaldo chini ya Rais Florentino Eduardo Pérez alisaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuichezea Real Madrid utakaomuweka klabuni hapo hadi 2021, na huku mkataba huo utamuwezesha kulipwa kiasi cha pound 365000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 900.
Ronaldo amesaini mkataba huo na kueleza malengo yake kuwa anataka kucheza soka hadi atakapo fikisha umri wa miaka 41 na anaamini atakuwa kafunga magoli mengi katika maisha yake ya soka.
“Leo ni siku muhimu kuongeza mkataba na klabu niipendayo ni kitu muhimu sana kuongeza mkataba wa miaka mitano, lakini naomba ieleweke huu sio mkataba wangu wa mwisho nataka kuweka historia kwa kufunga magoli na kushinda mataji zaidi”
CHRISTIANO RONALDO: YUPO REAL MADRID HADI 2021
Reviewed by Unknown
on
01:51
Rating:
No comments: