Recent Posts

SIMON MSUVA KUPOKEA ZAWADI NONO VPL.



 Simon Msuva ndiye mchezaji bora wa mwezi octoba katika ligi ya Vodacom.
Msuva anayechezea timu ya Yanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.ambapo amewashinda nyota wawili kutoka timu ya Simba ambao ni Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya ambaye ndiye aliyeibuka mchezaji bora mwezi uliopita.

Aidha mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).

Fahamu kupitia ushindi huo wa  tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye pia  alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
SIMON MSUVA KUPOKEA ZAWADI NONO VPL. SIMON MSUVA KUPOKEA ZAWADI NONO VPL. Reviewed by Unknown on 01:05 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.