ALIYEKUWA SPIKA WA BUNGE; SAMWELI SITTA AFARIKI DUNIA.
Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
Mzee Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo Tabora Samwel Sitta.
"Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.
Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu.
Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni” alisema Rais Magufuli.
Taarifa ya salamu za rambirambi imetolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU. Dar es Salaam.
*************************
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI....Amen!!

Reviewed by Unknown
on
00:23
Rating:
No comments: