Recent Posts

ALEX SANCHEZ ATUA RASMI ARSENAL ASAINI MIAKA MITANO

KLABU ya Arsenal imekamilisha usajiri wa mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona raia wa Chile Alex Sanchez kwa dau la paun million 30 na tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitano.

Nyota huyo wa Chile, ambaye alikatisha mapumziko yake mafupi kwenda kukamilisha uhamisho wake kutua London, amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wenye kipengele cha uwezekano wa kuongezewa miezi 12 ambao utamfanya alipwe mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki.

Kiwango hicho kitamfanya Sanchez mwenye miaka 25 alingane na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, kiungo Mesut Ozil aliyekuwa anaongoza kulipwa Gunners.

"Nina furaha mno kujiunga na Arsenal, klabu ambayo ina kocha babu kubwa, kikosi chenye wachezaji wazuri haswa, sapoti kubwa dunia nzima na Uwanja mkubwa mjini London," alisema Sanchez.

#By_Sports_Admin_Emmanuel_Senny



ALEX SANCHEZ ATUA RASMI ARSENAL ASAINI MIAKA MITANO ALEX SANCHEZ ATUA RASMI ARSENAL ASAINI MIAKA MITANO Reviewed by Unknown on 08:48 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.