Moja ya Wasanii wakongwe wa Hip-hop ni Busta Rhymes Fahamu tu kuwa Mwanzo wa mwezi huu aliachia wimbo aliomshirikisha Eminem unaoitwa ‘Calm Down’, na sasa hivi anajiandaa kuachia albam yake mpya inayoitwa "E.L.E.2" ambapo kwa mfululizo wa albamu zake hii itakuwa ni Albamu ya Kumi.
Kwa mujibu wa Rap-Up.com Busta Rhymes ametangaza kujiondoa katika label ya YMCMB baada ya kuona kuwa amefanya kazi kwa takribani zaidi ya miaka miwili katika label hiyo pasipo mabadiliko ya kimaendeleo.
Busta ameweka wazi uamuzi huo wakati akihojiwa na SiriusXM katika kipindi cha Sway in The Morning kupitia MTV NEWS huku akitoa sababu kubwa kuwa ni kitendo cha maelewano kuwa hafifu katika utendaji wa kazi kiujumla.
Busta alitangaza kujiunga na Cash Money November, 2011 ingawa hajawahi kuachia albam akiwa ndani ya label hiyo, hata hivyo Busta Rhymes pia aliwahi kuingia katika label ya Dr Dre na kushindwa kudumu kwa muda mrefu japo hakuwahi kutangaza sababu kubwa ya kuondoka kwake katika label hiyo.
“Nothing happened in a negative way, I was there for two years and the opportunity was a great opportunity at the time because of the type of deal that was done. For me, with this particular project and all of the sacrifice that went into it—recording the album for five years, If I feel like, in the slightest way, we ain’t facilitating everything necessary for the vision to be seen and executed in the way I’m envisioning this shit for the last five years, let me live and die in my own own inequity, homie,” alisema Busta Rymes.
Hata hivyo Busta Rymes alisema ameongea na Bird Man ambaye ni Founder wa Cash Money juu ya suala la kutoa na kufanya naye kazi za baadae na alisema kuwa hilo halina tatizo ingawa hata kuwa tena ndani ya label hiyo.“After I see this through, if there’s other opportunities for us to explore as businessmen together, let’s continue to do it.” ndivyo alivyo ambiwa na Bird Man.
BUSTA RYMES AJITOA CASH MONEY NA HIZI NDIO SABABU ZAKE!!.
Reviewed by Unknown
on
01:12
Rating:
No comments: