Recent Posts

JORDAN YAUMIZWA NA MAUAJI YA MUANDISHI.

JORDAN YAUMIZWA NA MAUAJI YA MUANDISHI.

Mfalme Abdullah wa Jordan aliyalaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Japan yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la islamic state.

Mfalme huyo aliyaita mauaji hayo ya Kenji Goto kuwa ni tendo la kihalifu na kuongeza kuwa juhudi zilifanywa kuweza kuachiwa huru kwa Rubani raia wa Jordan ambae anashikiliwa na kundi hilo la wapiganaji.

Maafisa wa usalama nchini Jordan walisema kuwa wamekuwa wakijaribu kufahamu kama rubani huyo Muath al- kasaesbeh yuko hai au ameshafariki.

Msemaji wa serikali alisema kuwa Jordan ilikuwa na nia ya kumuachia huru mwanachama wa Al- qaeda,mlipuaji bomu sajida al Rishawi huru kwa rubani huyo.

Iliripotiwa kuwa Jordan imekuwa ikifanya mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi wa kikabila kwa rubani huyo.

JORDAN YAUMIZWA NA MAUAJI YA MUANDISHI. JORDAN YAUMIZWA NA MAUAJI YA MUANDISHI. Reviewed by Unknown on 05:49 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.