Recent Posts

NEWS: MASHOGA WANYANYASWA.

MASHOGA WANYANYASWA.

Wakereketwa wa haki za binadamu nchini Uganda walishutumu polisi wa nchi hiyo kwa kuwanyanyasa
na kuwapiga wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Katika hatua hiyo kundi liitwalo chapter Four Uganda lilisema kuwa limeorodhesha visa kadhaa
ambavyo polisi wanawalizimisha wanaume kuvua nguo zao na kubaki bila ya nguo ili kuonyesha
sehemu zao nyeti kubaini iwapo wanahusika katika matendo hayo ya ngono ya jinsia moja.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Uganda Jenerali Aronda Nyakairima aliiambia BBC kuwa madai hayo
si ya kweli na alisema kuwa ofisi yake itachunguza.

Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini Uganda hata hivyo serikali ina mpango wa kuanzisha sheria
kali zaidi.

NEWS: MASHOGA WANYANYASWA. NEWS: MASHOGA WANYANYASWA. Reviewed by Unknown on 07:27 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.