MTANGAZAJI WA BBC AWADHALILISHA WATU "63".
Uchunguzi uliofanyika kiundani zaidi kuhusu mtangazaji wa zamani wa shirika la utangazaji la "BBC" maarufu sana hapa duniani Jimmy Savile, umebaini kuwa Savile aliwazalilisha watu wapatao
63 kutoka hospitali ya Stoke mandeville nchini
uingereza huku malalamiko rasmi yaliyotolewa kutokana na vitendo vyake vya kupenda Ngono.
Hatua hiyo ya uchunguzi ulibaini kuwa sifa ya Savile kama mpenda ngono ilikuwa ikifahamika miongoni
mwa baadhi ya wafanyakazi,lakini tuhuma hizo huenda hazikuwafikia viongozi.
Malalamiko rasmi yaliyotolewa mwaka 1977 na baba
wa muathirika aliyetakiwa kuripotiwa polisi.
Hata hivyo ripoti hiyo ilisema kuwa matendo ya habari ya Savile yangeweza kutokea tena,sambamba
na hayo ripoti ya stoke mandaville ilisema kuwa waathirika walidhalilishwa kutoka miaka minane hadi 40.
No comments: