MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA.
Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika
Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita,
alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka
ghafla na baadaye kidogo alifariki" alisema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Aidha Katibu wa mbunge huyo Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika
hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Sambamba na hayo Gaspaer ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
No comments: