RAISI JAKAYA KIKWETE YUPO NCHINI ZAMBIA KWA
KUIJADILI "TAZARA".
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete aliondoka nchini jana
kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya ziara ya kikazi
ya siku mbili kutokana na mwaliko kutoka kwa Raisi
wa nchi hiyo Edgar Chagwa Lungu pamoja na
kujadili changamoto mbalimbali zinazoikumba reli
inayounganisha Tanzania na Zambia"Tazara".
Kwa mujibu wa taarifa ya kutoka kwa mwandishi wa habari wa Raisi, msaidizi Premu Kibabgu,alisema kuwa viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili swala kubwa likiwa kujadili reli.
Kibabgu alisema kuwa reli ya Tazara katika siku za hivi karibuni ilikuwa ikikabiliwa na changamoto
mbalimbali ambazo zilihitaji kujadiliwa kwa kina na viongozi wakuu ili kuimarisha zaidi reli hiyo ambayo ni kiungo kikubwa baina ya nchi hizi katika masuala
ya uchumi na alama ya ushirikiano.
Tazara ilizinduliwa rasmi Oktoba 1975,Kwa ufadhili wa china na ina upana wa milimita 1067 na urefu wa kilometa 1860 kuanzia Dar es salaam, Tanzania na kuishia katika mji wa uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani milioni 5 na watu milioni 3 kwa mwaka.
No comments: