Recent Posts

CHILE KUIVAA ARGENTINA FAINALI YA COPA AMERICA

>>
Wenyeji wa kombe la Copa America Chile wamefuzu kufika fainali mara ya kwanza kwa miaka 28. Hii ni baada ya kuwanyuka Peru mabao mawili kwa moja katika mchuano uliofanyika mjini Santiago.

Nusura kiungo wa kati wa Chile Arturo Vidal kuondolewa mapema, hata hivyo bahati mbaya ilikua wa mlinda lango wa Peru Carlos Zambrano aliyepewa kadi nyekundu.
Eduardo Vargas alisaidia timu yake kupata magoli mawili

Aliyekua mshambuliaji wa klabu wa QPR ya Uingereza Eduardo Vargas alisaidia Chile kupata bao la kwanza dakika ya 42.

Hata hivyo Peru ilisawazisha pale Gary Medel alipojifunga bao. Vargas ndiye aliipatia Chile bao la pili na la ushindi katika dakika ya 64.

Chile haijawahi kushinda kombe la Copa kwa karibu karne moja. Chile wanaingia fainali hapo Jumamosi ambapo watapambana na Argentina ambayo iliitoa Paraguay kwa jumla ya mabao 6-1.
CHILE KUIVAA ARGENTINA FAINALI YA COPA AMERICA CHILE KUIVAA ARGENTINA FAINALI YA COPA AMERICA Reviewed by Unknown on 16:07 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.