Maafisa wa serikali Kaskazini mwa Nigeria wamesema kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio la bomu la kujitolea mhanga katika mji wa Zaria.
Ripoti zilisema kuwa watu wengine wengi wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulio hilo lilitokea katika jengo moja la serikali ambako wafanyakazi wa serikali walikuwa wamekusanyika kusajiliwa.
Wengi waliokuweko katika jengo hilo ni walimu na wafanyikazi wa umma.
Katika kipindi cha majuma 2yaliopita takriban watu 220 wameuawa katika mashambulizi kadha yanayolaumiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Gavan wa jimbo la Kaduna amewaonya wenyeji kuwa waangalifu sana na kuepuka maeneo
yaliyojaa watu kwani hayo ndio yanayolengwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga.
WATU 20 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA SHAMBULIO.
Reviewed by Saidia Turuki
on
06:14
Rating:
No comments: