Klabu ya Manchester Utd imekamilisha usajiri wa Kipa Sergio Romero, aliyekuwa
akiichezea klabu ya Sampdoria, na amejiunga na vijana wa Louis Van Gaal
baada ya kukamilisha muda wa mkataba wake na Sampdoria.
Kipa huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu na anatarajiwa kuchukua nafasi ya kipa wa akiba, Victor Valdes ambaye ameambiwa yuko huru kuihama klabu hiyo na Van Gaal.
Romero alikuwa katika timu ya taifa ya Argentina iliyofika fainali ya Copa America mwaka huu na kombe la dunia nchini Brazil mwaka uliopita.
Kwa sasa kipa huyo ameungana na wana-devils katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo nchini Marekani.
Mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji waliofunzwa na Van gaal ambao wameungana naye Old Trafford wengine wakiwa ni Memphis Depay, na Daley Blind.
Hatua ya kumsaini Romero inaonekana ni kama njia ya kupiga jeki idara ya ulinzi katika Manchester United huku Mhispania, David De gea akiendelea kusakwa na ReaL Madrid.
SERGIO ROMERO ATUA MAN UTD
Reviewed by Unknown
on
04:48
Rating:
No comments: