Recent Posts

JOHN MNYIKA ASIMAMISHA KIKAO BUNGENI MKOANI DODOMA

Mbunge wa Ubungo jijini Dar es salaam, John Mnyika jana alisimamisha kikao cha bunge,na kumsababishia spika wa bunge Anna Makinda kusimamisha kikao hicho.

Mbunge huyo alitaka kujua baadhi ya vipengele vya bajeti,na kumwambia spika ajibu,na spika huyo alijibu na kusema hawezi kulazimishwa kuongea.

Ndipo John Mnyika aliposema hatoki bungeni mpaka apewe jibu sahihi la vipengele hivyo.

Sambamba na hayo na wabunge wengine nao walipoanza kusema kuwa hawatoki bungeni mpaka kieleweke huku wakipiga kelele.

Spika wa bunge alisitisha kikao cha bunge na kusema bunge litaendelea siku nyingine huku nyuma akizomewa.

JOHN MNYIKA ASIMAMISHA KIKAO BUNGENI MKOANI DODOMA JOHN MNYIKA ASIMAMISHA KIKAO BUNGENI MKOANI DODOMA Reviewed by Saidia Turuki on 06:15 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.